728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 05, 2016

    MICHAEL BALLACK YEYE NA OLIVIER GIROUD TU EURO 2016

    Munich, Ujerumani.

    KIUNGO wa zamani wa Chelsea,Mjerumani Michael Ballack,amesema mshambuliaji wa Ufaransa na Arsenal,Olivier Giroud,amemfanya awe shabiki wake mkubwa katika michuano inayoendelea ya Euro 2016.

    Ballack amemwagia sifa kemkem,Giroud,29,baada ya mshambuliaji huyo wa zamani wa Montipellier kutangazwa mchezaji bora wa mechi kufuatia kuifungia Ufaransa mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Iceland katika mchezo wa robo fainali uliochezwa siku ya Jumapili katika uwanja wa Parc de Princes.

    Ameiambia ESPN.“Labda hapati sifa nyingi baadhi ya nyakati kwa kuwa hana kasi sana.Lakini Giroud anajua sana kucheza mbele ya lango la wapinzani akiwa na mpira ama asipokuwa na mpira na hilo tumeliona katika mchezo  dhidi ya Iceland"  

    Amekuwa Mchezaji wangu kipenzi katika michuano hii Kwa sababu amekuwa anacheza katika namna ambayo mara zote amekuwa ikiisaidia timu kupata ushindi".Alimaliza Ballack.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MICHAEL BALLACK YEYE NA OLIVIER GIROUD TU EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top