728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 05, 2016

    CAF YAZIPIGA STOP YANGA SC,MEDEAMA FC KUCHEZA CCM KIRUMBA

    Cairo,Misri.

    NDOTO ya mashabiki wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kuiona timu yao ya Yanga SC ikicheza japo mchezo mmoja wa kombe la Shirikisho katika Uwanja wao wa CCM Kirumba imeota mbawa baada ya shirikisho la soka Afrika CAF kusisitiza kuwa mchezo dhidi ya Medeama FC ya Ghana uliopangwa kuchezwa Julai 16 ni lazima uchezwe katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na siyo vinginevyo.

    Taarifa hiyo ya CAF imekuja baada ya mapema wiki hii kuibuka kwa habari kuwa Yanga SC ilitaka mchezo huo uchezwe katika Uwanja wa CCM Kirumba wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 35,000 badala ya Uwanja wa Taifa.

    CAF kupitia kwa msemaji wake, Junior Binyam,imesema uwezekano wa mchezo huo kuchezwa CCM Kirumba haupo kwa kuwa uwanja huo haupo katika orodha ya viwanja vilivyoorodheshwa kutumika katika michuano hiyo.Uwanja unaotambuliwa na CAF ni ule wa Dar es Salaam na siyo CCM Kirumba.

    Kabla ya michuano ya shirikisho na ile ya klabu bingwa Afrika,CAF ilivifanyia ukaguzi viwanja vyote vilivyopendekezwa na vilabu ili kujiridhisha kama vina sifa ya kutumika katika michuano yake au la na Uwanja wa CCM Kirumba haukuwa sehemu ya viwanja hivyo.Hivyo mchezo huo utachezwa Dar es Salaam.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YAZIPIGA STOP YANGA SC,MEDEAMA FC KUCHEZA CCM KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top