Valencia, Hispania.
WINGA wa zamani wa vilabu vya Manchester United na Sporting Lisbon,Mreno Luis Carlos Almeida
da Cunha 'Nani' amejiunga na klabu ya Valencia ya Hispania akitokea klabu ya Fenerbahce kwa ada ya €8.5m.
Taarifa rasmi kutoka katika mtandao rasmi wa klabu ya Valencia imesema:
"Valencia inapenda kuwataarifu kuwa imefikia makubaliano ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ureno, CarlosAlmeida da Cunha 'Nani' (29) kwa misimu mitatu ijayo.Atajiunga na klabu yetu baada ya kumalizika kwa michuano ya Euro 2016".
Nani alijiunga na Fenerbahce mwaka 2015 akitokea Sporting Lisbon,akifanikiwa kucheza jumla ya michezo 46 na kuifunga mabao 12.
0 comments:
Post a Comment