Swansea,Wales.
KLABU ya Swansea City imetangaza kumsajili kiungo wa Uholanzi,Leroy Fer,kutoka Klabu ya QPR kwa ada ya £4.75m.
Fer,26,amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuitumikia miamba hiyo ya Liberty Stadium baada ya kocha wa klabu hiyo Muitaliano Francesco Guidolin,kupendekeza kiungo huyo wa zamani wa Norwich City asajiliwe kufuatia kuonyesha kiwango kizuri wakati akiitumikia klabu hiyo kwa mkopo msimu uliopita.
Fer anaiacha QPR baada ya kuifungia mabao manane katika michezo 50 ya michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu England, Capital One na FA Cup.
Aliwahi kufeli vipimo vya afya mara mbili!!
Fer amekuwa na bahati mbaya linapofikia zoezi la kufanyiwa uchunguzi wa afya yake ili ajiunge na vilabu vingine.
Mwaka 2013, Fer alishindwa kujiunga na Everton akitokea FC Twente ya nyumbani kwao Uholanzi baada ya vipimo kuonyesha kuwa alikuwa na tatizo katika goti lake.
Mwaka 2015 goti hilo hilo tena lilimnyima Fer nafasi ya kujiunga na Sunderland baada ya vipimo kuonyesha tena tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment