Paris,Ufaransa.
SHIRIKISHO la vyama vya Soka Barani Ulaya UEFA limetishia kuziondosha katika mashindano yanayoendelea ya Ulaya [Euro 2016] nchi za England na Urusi kama mashabiki wao wataendelea na vurugu.
UEFA imetoa onyo hilo kali baada ya Jumamosi usiku mashabiki wa England na Urusi kuchapana makonde katika mchezo wao wa kundi B ulioisha kwa timu zao za taifa kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
UEFA imevipa Onyo kali vyama vya soka vya England (FA) na Urusi (RFU) na kuvitaka viweze kuwadhibiti mashabiki wao vinginevyo timu zao za taifa zitaondolewa mashindanoni mara moja.
Katika vurugu hizo zilizoanzia ndani ya uwanja wa Stade Veledrome na kisha kuhamia nje katika mitaa ya mji wa Marseille ilishuhudiwa mashabiki wengi wakiumia na wengine kutiwa nguvuni na wanausalama huku pia uharibifu wa vitu mbalimbali ukiripotiwa kutokea.
Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwanza mashabiki wa Urusi ndiyo walioanzisha vurugu hizo baada ya timu yao kupata bao la kusawazisha dakika za lala salama.
0 comments:
Post a Comment