Washington,Marekani.
ARGENTINA na Chile zimefanikiwa kuwa timu pekee kutoka kundi D kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America Centenario baada ya Alfajiri ya leo kupata ushindi mkubwa dhidi ya Bolivia na Panama.
Argentina wakiwa katika dimba la CenturyLink Field, Seattle,huko Washington wameifunga Bolivia kwa mabao 3-0.Mabao hayo yametiwa kimiani na Erik Lamela 13',Ezequel Lavezzi 15' na msumali wa mwisho ukipigwa na Victor Cuesta 32'
Katika mchezo mwingine wa kundi D,Chile imeifunga Panama kwa mabao 4-2.Mabao ya Chile yamefungwa na Eduardo Vargas na Alexis Sanchez wote wamefunga mara mbili.Panama wao wamepata mabao yao kupitia kwa Miguel Camargo na Abdiel Arroyo
Ratiba ya robo fainali
Argentina vs Venezuela
Chile v Mexico
Marekani v Ecuador
Peru v Colombia
0 comments:
Post a Comment