Manchester,England.
Hatimaye mlinda mlango David De Gea amesaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kuichezea Manchester United.Mkataba huo mpya wenye nafsi ya kurefushwa utafikia tamati mwaka 2019 umesaini baada ya pande zote mbili kuridhia makubaliano baada ya kutokea kwa sintofahamu kufuatia Manchester United kumuwekea ngumu kuhama staa huyo.
Mkataba huo mpya utamuwezesha De Gea kuvuna kitita cha paundi milioni 10 kwa mwaka baada ya kuongezewa mshahara kutoka paundi 35,000 mpaka 200,000 kwa wiki na kuwa mlinda mlango anayelipwa zaidi kuliko walinda mlango wote duniani.
De Gea,24 alijiunga na Manchester United mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na kitita cha paundi milioni 17.Mpaka sasa De Gea ameshaichezea Manchester United jumla ya michezo 175.
0 comments:
Post a Comment