728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, September 11, 2015

    IMETOSHA SASA:ADEBAYOR KUTOICHEZEA TENA SPURS MAISHANI


    London,England.

    Msambuliaji Emanuel Adebayor hataweza tena kuichezea Tottenham Hotspurs baada ya kocha mkuu wa klabu hiyo Muargentina Mauricio Pochettino kutangaza rasmi leo kuwa nyota huyo wa Togo hayuko kwenye mipango yake ya msimu huu na mingine ijayo.

    Pochetino amesema hayo baada ya Adebayor,31 kukataa kujiunga kwa mkopo na vilabu vya Aton Villa na Westham United katika dirisha lililopita la usajili kwa madai kuwa alitaka alipwe paundi milioni 5 ili aachane jumla na Tottenham.

    Pochettino "Nilifanya nae mazungumzo mwishoni mwa msimu uliopita na nikamwambia kusudio langu.Sihitaji tena kurudia jambo hilo.Nafikiri hilo liko wazi.Hayuko katika mawazo yangu,katika akili yangu na katika mipango ya baadae ya Tottenham" 
    Kufuatia sakata hilo Adebayor ataendelea kuvuna bila jasho kitita cha paundi 100,000 ambacho ndiyo mshahara wake wa wiki katika klabu hiyo ya White Hatlane.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IMETOSHA SASA:ADEBAYOR KUTOICHEZEA TENA SPURS MAISHANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top