Arsenal imekuwa timu ya kwanza kutoka ligi kuu England kutangaza kuwa itatoa msaada kwa wakimbizi wa kivita katika nchi za mashariki ya kati na Afrika.
Arsenal itachangia £1 kwa kila tiketi moja itakayouzwa katika mchezo wake wa jumamosi dhidi ya Stoke City ili kuwasaidia wakimbizi wa Syria kutokana na taifa hilo kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Wakati huohuo shirikisho la vyama vya soka Ulaya (Uefa) lenyewe linatarajia kuchangisha jumla ya £2m baada ya raundi ya kwanza ya michezo ya Champions itakayopigwa wiki ijayo.Tayari vilabu vyote 80 vinavyoshiriki katika michuano hiyo vimekubali kutoa £1 kutoka katika kila tiketi moja itakayouzwa katika michezo hiyo.
Bayern Munich imekuwa klabu ya kwanza kutoka Ujerumani kuwachangia wahanga wa kivita baada ya kutoa kitita cha £720,000
0 comments:
Post a Comment