England imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ijayo ya mataifa ya Ulaya (Euro 2016) baada ya kuibuka na ushindi wa goli 6-0 dhidi ya San Marino katika mchezo uliopigwa jioni ya leo huko Marino.
England ilianza kujihakikishia ushindi dakika ya 13 kupitia kwa nahodha wake Wayne Rooney kabla ya Brolli wa Marino kujifunga dakika ya 30.England ilipata magoli mengine kupitia kwa Theo Walcott na Harry Kane ambao walifunga mara mbili kila mmoja.
Kufuatia ushindi huo mkubwa England imekata tiketi ya kuwemo katika michuano ijayo itakayofanyika huko Ufaransa mwakani.
Wakati huohuo mshambuliaji wa England Wayne Rooney ameifikia rekodi ya mkongwe Sir Bobby Charlton baada ya kufikisha magoli 49.
0 comments:
Post a Comment