Huston,Marekani.
Lionel Messi ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mwamba baada ya hapo juzi kutumia dakika 25 pekee kuifungia Argentina mabao mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Bolivia na kuweka rekodi ya kuwa Muargentina wa kwanza kufanikiwa kuzifunga timu zote za Amerika ya Kusini.
Messi aliyeingia dimbani dakika ya 65 akitokea benchi aliifungia Argentina mabao wawili katika ushindi wa bao 7-0 dhidi ya Bolivia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa huku Huston,Marekani.
Kufuatia mabao hayo mawili Messi amefikisha jumla ya mabao 48 yakiwa ni mabao manane pungufu ili aweze kumfikia mfungaji wa muda wote wa Argentina Gabriel Batistuta aliyeifungia Argentina "Albicelestes" jumla ya mabao 56 kabla ya kuachana na soka.
Rekodi hii mpya ya Messi ilikuwa iwekwe mapema na Gabriel Batistuta lakini mpaka anastaafu Batistuta hakuwahi kuifunga Ecuador pekee katika timu za ukanda wa Amerika ya Kusini.
0 comments:
Post a Comment