728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 04, 2015

    HOMA YA NGAO YA JAMII:AZAM FC YAIENDEA YANGA ZANZIBAR

     
    MABINGWA wapya wa Kombe la Kagame, Azam FC, wanatarajia kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga utakaochezwa Agosti 22, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    Azam FC wataondoka jijini Dar es Salaam wakiwa na kikosi kamili kujiandaa na mchezo huo wa kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

    Kikosi hicho kitakwenda kufanya maandalizi yake baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 5-3 katika mchezo wa robo fainali wa Kombe la Kagame kufuatia timu hizo kutofungana ndani ya muda wa kawaida wa dakika tisini.

    Hata hivyo, Azam FC walitawazwa mabingwa wapya wa kombe hilo baada ya kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


    Akizungumza jijini jana kocha mkuu wa timu hiyo, Stewart Hall, alisema amewapa mapumziko ya siku nne wachezaji wake ambapo Ijumaa watakutana na kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.


    Alisema Jumamosi kikosi chake kitasafiri kuelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi na kucheza michezo mitatu ya kirafiki, itacheza na KMKM, Mafunzo pamoja na Kombaini Zanzibar.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HOMA YA NGAO YA JAMII:AZAM FC YAIENDEA YANGA ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top