728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 04, 2015

    SIMBA,AZAM ZAMTOLEA NNJE STRAIKA WA KAGAME

                              
    Kama ilivyokuwa kwa Simba, Kocha Mkuu wa Azam, Mwingereza Stewart Hall, amesema straika wa Gor Mahia, Michael Olunga ni
    mzuri na angependa awe naye kikosini, lakini dau lake ni kubwa sana kiasi anaona ni bora ampotezee tu.

    Akizungumza Stewart alisema soka la Olunga linavutia, ikizingatiwa anasaka straika wa kigeni, lakini kwa dau analotaka Mkenya huyo wanaona bora waachane naye.

    “Mimi na benchi langu la ufundi tulivutiwa zaidi na straika huyo ambaye tunaamini kama tungemsajili angekuwa na faida kubwa kwenye kikosi chetu, ila tuliamua kuachana naye kwa vile bei yake ni kubwa na isiyolingana na uwezo wake.

    “Gor Mahia ilitaka fedha nyingi sana, jambo ambalo uongozi haukuafikiana nao. Thamani ya Olunga si kubwa kiasi hicho. Hakuna klabu yoyote Afrika Mashariki itaweza kumchukua kwa dau hilo,” alisema.

    Hata hivyo kocha huyo alisema kuwa anaangalia uwezekano wa kusajili wachezaji wengine walioonesha kiwango kikubwa kwenye michuano ya Kagame.

    Mwanzoni mwa Kagame, Simba ilirusha ndoano kwa Olunga, lakini dau kubwa liliwakimbiza sawa na ilivyo kwa Yanga na sasa Azam klabu inayotajwa kuwa tajiri nchini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIMBA,AZAM ZAMTOLEA NNJE STRAIKA WA KAGAME Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top