728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 04, 2015

    YANGA YALETA BEKI KISIKI MCAMEROON

     
    YANGA wameonyesha jinsi walivyopania kufanya kweli msimu ujao baada ya kumtwaa beki kisiki wa kati kutoka nchini Cameroon, Bate Takang,
    mwenye nguvu balaa na mwili mkubwa zaidi ya Muivory Coast wa Azam, Pascal Wawa.

    Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanajipanga kutetea ubingwa wao wa kipute hicho kilichopangwa kuanza Septemba 12, mwaka huu, lakini pia kutikisa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

    Takang anayetokea klabu ya Bhthere Sportif inayoshiriki Ligi Kuu Cameroon, tayari ametua ameanza mazoezi jana kwenye Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.

    Mcameroon huyo aliyetua nchini ikiwa ni siku mbili kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Bara, akifanikiwa majaribio yake anatarajiwa kumaliza tatizo la ulinzi katika kikosi cha Yanga.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YALETA BEKI KISIKI MCAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top