Klabu ya Arsenal imeripotiwa kujiandaa kumsajili mlinda mlango namba moja wa klabu ya Olympiacos Muhispania Roberto Jimenez.
Jimenez,29 aliyewahi pia kuichezea klabu ya Atletico Madrid kabla ya kuuzwa ameibuka katika orodha ya washika mitutu hao wa London [Arsenal] ili kuja kuongeza nguvu katika idara ya ulinda mlango kufuatia walinda mlango Wojciech Szczesny na Emiliano Martinez kuihama klabu hiyo kwa mkopo huku hatima ya mlinda mlango mwingine David Ospina ikiwa bado haijafahamika ikiwa atabaki na kuwa msaidizi wa Peter Cech ama nae ataondoka.
Msimu uliopita Jimenez alifanikiwa kuichezea Olympiacos jumla ya michezo 41 huku akifanikiwa kutoruhusu goli lolote katika nusu ya michezo aliyoicheza.
0 comments:
Post a Comment