London, England.
Maisha ya mlinda mlango Wojciech Szczesny ndani ya klabu ya Arsenal yameendelea kuwa magumu baada ya nyota huyo kulimwa faini nzito ya £20,000 kwa kosa la kuvuta sigara.
Szczesny alikutwa na kosa hilo bafuni muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Southampton katika dimba la St.Mary's ambapo Arsenal ililala kwa mabao 2-0 ambayo yalitokana na uzembe wa mlinda mlango huyo.
Kufuatia sakata hilo inasemekana kocha Arsenal Wenger alikasirika na kuamua kumuweka benchi mlinda mlango huyo katika mchezo uliopita wa kombe la FA dhidi ya klabu ya Hull City.
0 comments:
Post a Comment