London,England.
MWAMUZI Mark Clattenburg amejiuzulu kuchezesha ligi kuu England na muda wowote kuanzia sasa atatimkia nchini Saudi Arabia kwenda kuwa mkuu wa waamuzi.
Clattenburg mwenye umri wa miaka 41 amekubali dili la mwaka mmoja kwenda kuchukua nafasi ya mwamuzi wa zamani wa England Howard Webb aliyejiuzulu wadhifa huo siku 11 zilizopita.
Baadhi ya majukumu ya Clattenburg yatakuwa ni kuwanoa waamuzi,kuboresha mfumo wa uwamuzi pamoja na kuchezesha baadhi ya michezo ya ligi kuu ya Saudi Arabia.
Clattenburg alianza kuchezesha mpira mwaka 2000 wakati huo akiwa na miaka 25.Miaka minne baadae alipanda daraja na kuingia ligi kuu ambapo amehudumu kwa miaka 12 ya mafanikio.
0 comments:
Post a Comment