728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    YANGA SC KUWAKOSA NYOTA WAKE WATANO DHIDI YA AZAM FC KESHO JUMATANO


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara,YANGA SC, kesho Jumatano watawakosa nyota wao watano pale watakapojitupa katika dimba laUwanja wa Taifa,kuvaana na Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

    Nyota watakaokosekana kesho ni Kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu,Mabeki Juma Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’ wanaosumbuliwa na maumivu ya miguu na Kevin Yondani anayeumwa jicho.



    Kevin Yondani

    Aidha katika mchezo huo Yanga SC pia itamkosa kiungo wake mshambuliaji toka Zambia,Obrey Chirwa, anayesumbuliwa na goti huku kukiwa na habari njema kuwa Donald Ngoma atashuka dimbani baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Mo Bejaia kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

    Mchezo huo utakaoanza saa 10:00 Jioni utachezeshwa na mwamuzi Ngole Mwangole atakayekuwa akisaidiwa Joseph Bulali kutoka Tanga na Frank Komba kutoka Dar Es Salaam.Kamisaa atakuwa Peter Temu kutoka Arusha.

    Hii ni mara ya pili mfululizokwa Yanga SC na Azam FC kukutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii ambao huashiria ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu Bara.Timu hizo zilikutana mara ya mwisho msimu na Yanga SC kuibuka washindi kwa penati 8-7 baada ya suluhu ndani ya dakika 90.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC KUWAKOSA NYOTA WAKE WATANO DHIDI YA AZAM FC KESHO JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top