728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    LIGI YA MABINGWA AFRIKA:ZAMALEK YAINYUKA ENYIMBA NA KUFUZU NUSU FAINALI BAADA YA MIAKA 11


    Cairo,Misri.

    MIAMBA wa soka wa Misri,Zamalek,wamefuzu nusu Fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika baada ya Jumatatu Usiku kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Miamba wa Nigeria,Enyimba International,katika mchezo mkali wa kundi B uliochezwa katika uwanja wa Petrosport Stadium huko jijini Cairo,Misri.

    Zamalek ambayo iliingia katika mchezo huo ikihitaji sare yoyote ile ili iweze kusonga mbele ilijipatia bao lake pekee na la ushindi dakika ya 63 ya mchezo baada ya Bassem Morsi kufunga kwa mkwaju wa penati.Bassem Morsi pia ndiye aliyefunga bao katika mchezo wa kwanza uliochezwa Nigeria ambao Zamalek pia waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

    Hii imekuwa ni mara kwanza kwa Zamalek kupenya mpaka hatua ya nusu fainali (Nne Bora) baada ya kujaribu bila mafanikio tangia mwaka 2005.

    Timu nyingine ambayo imefuzu nusu fainali kutoka kundi hilo la B ni vinara Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini

    Timu zilizofanikiwa kufuzu nusu fainali ni Mamelodi

    Sundowns ya Afrika Kusini na Zamalek ya Misri kutoka kundi B.Kutoka kundi B ni Wydad Athletic Club ya Morocco na Zesco United ya Zambia.

    Michezo ya nusu fainali itachezwa mwezi Septemba na itakuwa ya mikondo miwili ya nyumbani na ugenini,mchezo wa fainali pia utachezwa kwa utaratibu huo huo.

    Ratiba ya Nusu Fainali.

    Mamelodi Sundowns v Zesco/Wydad

    Zamalek v Zesco/Wydad

    IKUMBUKWE:Kundi A lenye Zesco United na Wydad linahitaji mchezo wa mwisho ili kujua timu ipi imeshika nafasi ya kwanza na ipi ya pili ila zote zimeshafuzu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA AFRIKA:ZAMALEK YAINYUKA ENYIMBA NA KUFUZU NUSU FAINALI BAADA YA MIAKA 11 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top