728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    ARSENAL YAMGEUKA MUSTAFI,YAGOMA KUONGEZA DAU,YAWAGEUKIA MABEKI WAWILI WA BEI CHEE


    Shrokdan Mustafi

    London,England.

    ARSENAL ni kama imemgeuka,Shrokdan Mustafi,hii ni baada ya kuripotiwakukataaa kutoa dau la £25m ambalo linatakiwa na klabu yake ya Valencia na badala yake inang'ang'ania kutoa dau la £20m ambalo tayari limewekewa ngumu.

    Kutoka Sky Sports habari zinasema kama dau hilo litaendelea kuwekewa ngumu basi Arsenal itawageukia mabeki Omer Toprak wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani na Simon Kjaer wa Fenerbahce ya Uturuki ambao wanapatikana kwa bei chee.




    Omer Toprak 

    OMER Toprak,27,alijiunga na Bayer Leverkusen mwaka 2011 akitokea Freiburg mpaka sasa ameichezea klabu hiyo michezo 103 ya ligi ya Bundesliga.Pia ameichezea timu yake ya taifa ya Uturuki jumla ya michezo 23 na alikuwa sehemu ya kikosi hicho kilichoshiriki michuano ya Euro 2016 iliyoisha mwezi Julai.

    Sifa yake kubwa ni Kiongozi mzuri ndani na nje ya uwanja pia inasemekana kuwa ana jicho kali la kuusoma mchezo.



    Simon Kjaer

    SIMON Kjaer,25,alijiunga na Fenerbahce msimu uliopita kwa ada ya £6.6m akitokea Lille ya Ufaransa na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo 28 ya ligi ya Uturuki na ile ya Ulaya.Ni raia wa Denmark.

    Sifa yake kubwa:Kjaer anasifika kwa kucheza soka la kibabe.Ni mzuri katika kufanya tackling pia ni mahiri katika kucheza mipira ya kutenga (set pieces) tatizo ambalo Arsenal wameshindwa kulipatia dawa.

    WAKATI HUOHUO habari za ndani zinasema Arsenal inataka kusajili beki mmoja wa bei chee ili pia ibaki na pesa ya kusajili mshambuliaji mmoja mpya kabla dirisha la usajili barani Ulaya halijafungwa mwezi huu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAMGEUKA MUSTAFI,YAGOMA KUONGEZA DAU,YAWAGEUKIA MABEKI WAWILI WA BEI CHEE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top