728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    BURNLEY YAMSAJILI DEFOUR KWA DAU LA REKODI


    Burnley,England.

    Klabu ya Burnley ambayo imerejea ligi kuu nchini England mchana huu imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo wa Ubelgiji,Steven Defour kutoka klabu ya RSC Anderlecht kwa dau la rekodi la £7.35m (€9m).

    Defour,28,amesaini mkataba wa miaka mitatu na anakuwa mchezaji wa nne kujiunga na Burnley inayonolea na Kocha Sean Dyche.

    Kabla ya kujiunga na RSC Anderlecht,Defour,aliwahi kuvichezea vilabu vya Genk na Standard Liege vya nyumbani kwao Ubelgiji kabla ya kutimkia Ureno na kujiunga na FC Porto aliyoisaidia kutwaa vikombe viwili vya ligi kuu.

    Defour ameichezea timu yake ya taifa ya Ubelgiji jumla ya michezo 46.Kabla ya kumsajili Defour Burnley hakuwahi kisajili mchezaji kwa dau la £7m hiyo usajili wa kiungo huyo ndiyo mkubwa zaidi kufanya na klabu hiyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BURNLEY YAMSAJILI DEFOUR KWA DAU LA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top