728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 10, 2016

    VIINGILIO YANGA,MO BEJAIA VYATAJWA CHA CHINI BUKU TATU



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    VIINGILIO vya mchezo wa marudiano wa Kundi A wa michuano ya kombe la Shirikisho kati ya wenyeji,

    Yanga SC ya Tanzania dhidi Mo bejaia ya Algeria utakaochezwa Jumamosi Agosti 13,2016 vimetajwa hii leo ambapo kiingilio cha chini kabisa kitakuwa Sh 3,000 kwa majukwaa ya

    mzungunguko.

    Kwa mujibu wa Waratibu wa Yanga viingilio vingine ni kuwa Viti Maalumu vyenye hadhi ya daraja B na C kiingilio kitakuwa Sh 10,000 wakati A kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000. 

    Mchezo wa Yanga dhidi ya Mo Bejaia utachezeshwa na waamuzi kutoka Ethiopia ambako katikati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa akisaidiwa na Kindie Mussie mstari upande wa kusini na Temesgin Samuel Atango katika mstari wa Kaskazini upande wa wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Haileyesus Bezezew Belete.

    Kamishna wa mchezo atakuwa Gaspard Kayijuka kutoka Rwanda wakati Desire Gahuka wa Burundi atasimamia ufanisi wa waamuzi wa mchezo na Mratibu Mkuu wa mchezo atakuwa Isam Shaaban kutoka Sudan.

    Mratibu huyo anatarajiwa kuwasili leo Agosti 10, 2016 wakati waamuzi watatua kesho Agosti 11, 2016 na msimamizi wa waamuzi atatua Ijumaa Agosti 12, 2016.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VIINGILIO YANGA,MO BEJAIA VYATAJWA CHA CHINI BUKU TATU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top