728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, August 11, 2016

    SWANSEA CITY YAMNASA STRAIKA WA ATLETICO MADRID KWA DAU LA REKODI


    Swansea,Wales.

    KLABU ya Swansea City leo imevunja rekodi yake ya usajili baada ya kufanikiwa kumsajili Straika,Borja Baston,kutoka klabu ya Atletico Madrid kwa ada ya £15.5m.

    Borja,23,ambaye msimu uliopita alifunga mabao 18 katika michezo 36 akiwa na klabu ya Eibar kwa mkopo amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Swansea City na atakuwa akivalia jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na Andre Ayew aliyehamia Westham United mwanzoni mwa wiki hii.

    Uhamisho huo umemfanya Borja kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya klabu ya Swansea City akivuka dau la £12m lililotolewa mwaka 2013 na klabu hiyo kumsajili Straika Wilfried Bony kutoka Vitesse Arnhem ya Uholanzi.

     Borja anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Swansea City katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.Wengine ni Leroy Fer (Queens Park Rangers),Mike van der Hoorn (Ajax), Mark Birighetti (Newcastle Jets) na Fernando Llorente (Sevilla).









    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SWANSEA CITY YAMNASA STRAIKA WA ATLETICO MADRID KWA DAU LA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top