728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 12, 2016

    OLIMPIKI:NIGERIA YASONGA ROBO FAINALI LICHA YA KUDUNDWA 2-0 NA COLOMBIA


    Manaus,Brazil

    NIGERIA imetinga robo fainali ya michuano ya Olimpiki kwa upande wa soka la wanaume licha ya Alhamis Usiku kufungwa mabao 2-0 na Colombia katika mchezo mwisho wa kundi B uliochezwa katika uwanja wa Amazonia Arena huko Manaus,Brazil.

    Colombia imepata mabao yake kupitia kwa Teofilo Guitierrez aliyefunga bao la kwanza dakika ya 4 ya kipindi cha kwanza na bao la pili limefungwa na Dorlan Pabon dakika ya 63 ya kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati

    Kwa matokeo hayo Nigeria ambayo imempoteza mshambuliaji wake hatari Oghenekaro Etebo kutokana na majeruhi imemaliza ikiwa kileleni mwa kundi B na itavaana na Denmark katika hatua ya robo fainali huku Colombia waliomaliza katika nafasi ya pili wakipata miadi ya kukutana na wenyeji Brazil.


    Katika mchezo mwingine wa kundi B,Japan imeifunga Sweden kwa bao 1-0 lililofungwa na Shinya Yajima.Kwa matokeo hayo Sweden na Japan zimefungasha virago kurudi nyumbani baada ya kumaliza zikiwa na pointi chache kuliko Nigeria na Colombia.







    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OLIMPIKI:NIGERIA YASONGA ROBO FAINALI LICHA YA KUDUNDWA 2-0 NA COLOMBIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top