Bastia,Ufaransa.
MABINGWA wa Ufaransa,Paris Saint-Germain,wameanza vyema kuutetea ubingwa wao baada ya leo usiku kuichapa timu ngumu ya Bastia kwa bao 1-0 katika mchezo mkali na mgumu uliochezwa huko Coriscan,Bastia.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 73 kwa mkwaju mkali na beki wa kushoto Layvin Kurzawa baada ya kipa wa Bastia,Jean-Louis Leca,kuutema mkwaju wa Jese Rodriguez.
Katika mchezo mwingine uliochezwa usiku huu Monaco na Guingap zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment