Jesse Jackson Were
Alexandria,Misri.
MABAO mawili ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Kenya,Jesse Jackson Were,yametosha kuipa Zesco United sare ya mabao 2-2 dhidi ya Al Ahly katika mchezo Mkali wa Kundi A wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Ijumaa Usiku katika Uwanja wa Borg El Arab huko Alexandria,Misri.
Were aliifungia Zesco United mabao hayo dakika za 6 na 35 huku yale ya wenyeji Al Ahly yakifungwa na Rami Rabia dakika ya 30 na Emad Moteab dakika ya 85.
Matokeo haya yanaiweka Zesco United kileleni mwa kundi A ikiwa na alama nane baada ya kushuka dimbani mara tano,Wydad Casablanca wako nafasi ya pili na alama saba katika michezo minne,Al Ahly ni wa tatu wakiwa na alama tano katika michezo mitano na mkiani wako ASEC Mimosas wenye alama nne katika michezo minne.
Sasa hii ina maana kwamba kama Waydad Casablanca wataifunga ASEC Mimosas Jumapili,Al Ahly watakuwa wametupwa rasmi nje ya michuano hiyo hata kama watashinda mchezo wao wa mwisho.
VIKOSI
Al Ahly XI: Adel, Fathi, Rabia, Samir, Rahil,Ashour, Ghaly, Zakaria, El-Said, Maaloul,Gamal.
Zesco United XI: Banda, Silwimba, Oluwafemi,Bahn, Odhiambo, Chaila, Mtonga, Chama,Chingandu, Mwanza,Were
0 comments:
Post a Comment