Dar es Salaam,Tanzania.
YANGA SC itamkosa Mshambuliaji wake hatari,Mzimbabwe Donaldo Ndombo Ngoma,katika mchezo wake wa marudiano wa kundi A wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.
Ngoma,26,alifikisha idadi hiyo ya kadi za njano Jumanne iliyopita wakati Yanga SC iliposhuka dimbani huko Sekondi-Tokoradi (Ghana) kuvaana na wenyeji wao Medeama FC.
Hii ina maana kwamba sasa safu ya ushambuliaji ya Yanga SC itawategemea Mrundi Hamis Tambwe,Watanzania Malimi Busungu,Matheo Antony na Mzambia Obrey Chirwa kuhakikisha kuwa inapata ushindi katika mchezo huo.
Yanga SC inatarajia kuvaana na Mo Bejaia Agosti 13, mwaka huu, katika Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment