728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 01, 2016

    NAMIBIA MABINGWA WAPYA COSAFA YA VIJANA

    Mauritius

    Namibia imetwaa ubingwa wa COSAFA 2016 kwa upande wa michuano ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 hii ni baada ya kuifunga Afrika Kusini kwa penati 3-1 kufuatia sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

    Bao la Namibia limefungwa na Godwin Awaseb dakika ya 64 huku lile la Afrika Kusini likifungwa na Thabiso Monyane dakika ya 70 na kufanya mchezo huo uende katika dakika za nyongeza na hatimaye kufikia hatua ya penati na Namibia kuibuka na ushindi.

    Mchezo huo pia ulitanguliwa na mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu na nne ambapo Malawi imefanikiwa kutwaa nafasi ya tatu katika michuano hiyo baada ya kuwafunga vijana wenzao wa Kenya kwa jumla ya mabao 2-0 yaliyofungwa na Peter Banda dakika ya 58 ambaye ameibuka mfungaji bora baada ya kupachika mabao matano.Bao jingine limefungwa na Francisco Madinga dakika ya 87.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NAMIBIA MABINGWA WAPYA COSAFA YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top