London,England.
WAMECHOKA!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuelezea hasira walizonazo kwasasa mashabiki wa Arsenal baada ya kuibuka taarifa kuwa klabu yao inataka kumsajili beki wa zamani wa Manchester United,Jonny Evans,ili kuchukua nafasi ya beki wao mkongwe Per Mertesacker ambaye ni majeruhi.
Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii hasa twitter wameponda mpango wa kumsajili beki huyo ambaye kwasasa anaichezea klabu ya West Bromwich Albion wakisisitiza kuwa siyo mchezaji sahihi wala hana ubora wa kuitumikia klabu hiyo.
Badala yake wameutaka uongozi wa klabu hiyo ukishirikiana na Kocha Arsene Wenger kuachana na mpango huo na kutafuta beki mwingine na siyo Evans anayedaiwa kuwa na thamani ya Paundi Milioni 16.
Baadhi ya mashabiki hao wamediriki kwenda mbali zaidi na kusema kuwa iwapo klabu hiyo itapuuza mawazo yao na kumsajili beki huyo basi wataisusa timu hiyo.Watafanya fujo,wataandamana na hata kuchoma bidhaa mbalimbali za klabu hiyo wanazozimiliki kama skafu na jezi.
Hii ni mara ya pili kwa mashabiki wa Arsenal kuijia juu klabu yao katika kipindi kama hiki cha usaji.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2014 pale alipozima jaribio la klabu yao kumsajili aliyekuwa kiungo wa Manchester United Tom Cleverly kwa kubadilishana na nahodha wao wa zamani Mbelgiji,Thomas Vermarlen.
0 comments:
Post a Comment