Dar es Salaam,Tanzania.
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa ameahirisha kambi ya timu hiyo iliyokuwa ianze Dar es Salaam leo.
Taarifa kutoka kwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas kwa waandishi wa habari jana ilisema kocha Mkwasa ameamua kuahirisha kambi hiyo baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu.
“Kutokana na maombi ya klabu nyingi za Ligi Kuu kutaka kuandaa wachezaji kwa ajili ya msimu unaoanza sasa,umemlazimu Kocha Mkuu timu ya Mpira Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa kuahirisha kambi iliyokuwa ianze Jumatatu Agosti mosi,” ilisema taarifa hiyo ya Lucas. Klabu za Ligi Kuu zinazoongoza kuwa na
wachezaji wengi kwenye timu ya taifa ni Simba,Yanga, Azam FC na Mtibwa Sugar.
Taarifa hiyo ilisema kutokana na hilo, Mkwasa atakuwa akifuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki ya klabu hizo inayofanyika kwa ajili ya maandalizi ya kuanza msimu mpya.
Taifa Stars inatarajiwa kucheza Lagos, Nigeria Septemba 2 mwaka huu katika mechi ya makundi kuwaniakufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika itakayofanyika Gabon mwakani. Hata hivyo mechi hiyo ni kama kukamilisha ratiba kwani Stars haina uwezo wa kufuzu kwenye kundi lake baada ya Chad
kujitoa na hivyo kubaki timu tatu.
Kundi hilo lilikuwa na timu za Tanzania, Chad, Nigeria na Misri ambayo ndiyo iliyofuzu michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment