728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 10, 2016

    NIGERIA YAPATA KOCHA MPYA NI MJERUMANI GERNOT ROHR


    Abuja,Nigeria.

    CHAMA cha soka cha Nigeria,NFF,kimemtangaza Mjerumani,Gernot Rohr,kuwa kocha mkuu mpya wa timu yake ya taifa ya Super Eagles kwa mkataba wa miaka miwili. 

    Rohr,63,aliyewahi kuzinoa timu za taifa za Gabon, Niger,Burkina Faso na vilabu vya Nantes,Nice,Young Boys Berne,Etoile du Sahel na Girondins Bordeaux atakuwa akisaidiwa na Salisu Yusuf na jukumu lao kubwa litakuwa ni kuhakikisha Nigeria inafuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 huko nchini Urusi.

    NFF iliamua kumgeukia  

    Rohr baada ya mwezi uliopita kushindwa kufikia makubaliano na Mfaransa,Paul Le Guen ili kuja kuchukua nafasi ya mzawa Sunday Oliseh aliyejiuzulu mapema mwezi Februari.

    Rohr ataanza kibarua cha kuinoa Nigeria hivi karibuni wakati miamba hiyo ya Afrika Magharibi itakapokuwa katika jiji la Port Harcourt kucheza na Tanzania katika mchezo wa kundi G wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2017 huko nchini Gabon.

    Historia fupi!!

    Mwaka 2012,Rohr,aliifikisha Gabon katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika (AFCON) iliyofanyika nchini humo kabla ya mwaka 2013 kujiunga na Niger na kisha Burkina Faso aliyoiongoza mpaka hatua ya mwisho ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NIGERIA YAPATA KOCHA MPYA NI MJERUMANI GERNOT ROHR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top