Dar es Salaam,Tanzania.
Simba SC sasa itacheza na AFC Leopards kutoka Kenya katika tamasha lake la Simba Day badala ya klabu ya Interclube ya Angola kama ilivyokuwa imetaarifiwa hapo kabla.
Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia mabadiliko ya ratiba huko nchini Angola yaliyopelekea klabu ya Interclube kutokuwa na nafasi ya kucheza mchezo huo ambao pia ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha miaka 80 ya uhai wa klabu ya Simba SC iliyoasisiwa mwaka 1936.
Tamasha hilo litafanyika tarehe 08/08 katika Uwanja wa taifa,Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment