728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 03, 2016

    CHELSEA YAMUUZA RASMI MOHAMMED SALAH

    Roma,Italia.

    Chelsea imemuuza rasmi winga wake raia wa Misri,Mohamed Salah,kwenda AS Roma baada ya klabu hiyo ya Italia kutoa kitita cha €15m.

    Salah,24, alijiunga na Chelsea Januari 2014 akitokea FC Basel ya Uswisi lakini alijikuta akipata wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza.

    Akiambulia kucheza michezo 19 pekee hali iliyomlazimu kujiunga na Fiorentina kwa mkopo wa msimu mmoja kisha baadae AS Roma katika msimu wa 2015/16.

    Akiwa na AS Roma,Salah,aliifungia klabu hiyo mabao 23 na kuiwezesha kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini Italia maarufu kama Seria A.

    Akiongea baada ya kukamilisha usajili huo Rais wa AS Roma,James Pallotta,amesema anataka kuifanya klabu hiyo iyafikie mafanikio ya vilabu vya Leicester City, Atletico Madrid na Sevilla ambavyo vimetwaa mataji kwa kutumia bajeti ndogo.

    Chelsea nao kwa upande wapo wamemshukuru Salah kwa mazuri aliyoifanyia klabu yao na wamemtakia mema huko aendako.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YAMUUZA RASMI MOHAMMED SALAH Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top