Leceister,England.
MABINGWA wa Ligi Kuu nchini England,Leicester City,wameendelea kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimuujaao baada ya mchana wa leo kumsajili winga,Bartosz Kapustka kutoka Cracovia ya Poland.
Kapustka,19,amesaini kandarasi ya miaka mitano baada ya kufuzu zoezi la upimaji wa afya yake.
Leicester City imeamua kumsajili Kapustka baada ya kuvutiwa na uwezo mkubwa aliouonyesha msimu uliopita akiwa na Cracovia hali iliyopelekea ajumuishwe katika kikosi cha Poland ambacho kilifika hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 iliyofanyika nchini Ufaransa.
Kapustka anakuwa mchezaji wa tano kujiunga na Leceister City baada ya Luis Hernandez,Ron-Robert Zieler, Papy Mendy na Ahmed Musa.
0 comments:
Post a Comment