Shalke,Ujerumani.
HATIMAYE mlinzi wa kushoto wa Ghana,Baba Rahman,ameihama Chelsea na kujiunga na Shalke 04 ya Ujerumani kwa mkopo wa msimu mmoja huku nyuma akiweka wazi kile kilichomuondoa katika klabu hiyo aliyojiunga nayo msimu mmoja uliopita.
Akifanya mahojiano na Ruhr Nachrichten,Rahman,22,amedai kuwa hakuwa na nafasi ya kuendelea kuichezea Chelsea mpya ya Muitaliano,Antonio Conte,kutokana na aina yake ya soka kuwa ya kushambulia zaidi na hivyo kutofautiana sana na ile ya kuzuia zaidi inayotaka kutumiwa na kocha huyo wa zamani wa Juventus.
Amesema "Conte anataka kikosi chake kicheze mchezo wa kuzuia zaidi,lakini mimi ni mlinzi ambaye aina yangu ya uchezaji ni ya kushambulia zaidi.
"Hivyo kama ningeendelea kubaki Chelsea ningekuwa na nafasi finyu sana ya kucheza chini ya Conte.Conte alinishauri kuondoka kwa mkopo.Tusubiri tuone nini kitakachotokea baada ya msimu huu.
Rahman alijiunga na Chelsea mwaka jana akitokea Augsburg kwa ada ya £17m lakini alijikuta akicheza michezo 23 pekee huku mingi kati ya hiyo akitokea benchi.
Wakati huohuo habari kutoka Ujerumani zinadai kuwa huenda Rahman asirudi tena Chelsea kwani Shalke 04 imepewa nafasi ya kumsajili moja kwa moja ikiwa itaridhishwa na kiwango chake.
jj
0 comments:
Post a Comment