728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 03, 2016

    MGHANA KEVIN PRINCE BOATENG APATA TIMU LA LIGA

    Madrid,Hispania.

    KIUNGO wa kimataifa wa Ghana,Kevin-Prince Boateng,amejiunga na Las Palmas inayoshiriki ligi daraja la kwanza Hispania maarufu kama La Liga kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru na kukabidhiwa jezi namba 7.

    Boateng,29,amejiunga na Las Palmas baada ya klabu ya AC Milan aliyoichezea msimu uliopita kushindwa kumpatia mkataba mpya kufuatia ule wa awali wa miezi sita kuwa umekwisha.

    Sababu za AC Milan kusita kumpa mkataba mpya staa huyo wa zamani wa vilabu vya Hertha Berlin,Tottenham, Borussia Dortmund, Portsmouth na Schalke ni kutokana na rekodi mpya ya majeruhi aliyonayo.

    Jumanne usiku mashabiki wapatano 5,000 wa Las Palmas walijitokeza katika dimba la Estadio Gran Canaria kushuhudia utambulisho wa kiungo huyo aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Ghana kilichofika robo fainali ya kombe la dunia la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

    Boateng amekuwa mchezaji wa nne kujiunga na Las Palmas katika dirisha hili la usajili barani Ulaya baada ya Helder Lopes, Marko Livaja na Michel Macedo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MGHANA KEVIN PRINCE BOATENG APATA TIMU LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top