Dar Es Salaam,Tanzania.
Yanga wanatarajia kufanya mkutano wa dharura wa wanachama uliopangwa kufanyika kesho Jumamosi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Yanga umeitisha mkutano huo wa dharura ikiwa ni siku chache tu baada ya Simba kuridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu yao Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit,alisema maandalizi ya mkutano huyo yamekamilika na unatarajia kuwa na ajenda sita.
Deusdedit alisema wanachama watapata fursa ya kujadili ajenda hizo ambazo zitawasilishwa na uongozi wa klabu hiyo.
Alitaja ajenda hizo kuwa ni mapato na matumizi ya klabu hiyo msimu uliopita na msimu mpya,marekebisho ya katiba katika baadhi ya vipengele, yatokanayo na mkutano wa mkuu wa uchaguzi,kuangalia ushiriki wa timu yao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uendeshaji wa klabu,udhamini wa klabu na mengineyo.
“Hizo ndizo ajenda kuu ambazo zitajadiliwa kwenye mkutano wetu, lakini kunaweza kuibuka nyingine kwenye mengineyo,”alisema.
Mkutano huo utakuwa wa kwanza tangu uongozi mpya wa klabu hiyo ulipoingia madarakani Juni 11 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment