Jeremy Peace
England.
UONGOZI wa West Bromwich Albion hivi punde umetangaza kuwa Mwenyekiti na Mmiliki wa klabu hiyo,Jeremy Peace,amefikia makubaliano ya kuiuza klabu hiyo kwa wawekezaji toka nchini China kampuni ya Yunyi Guokai (Shanghai) Sports Development Limited inayoongozwa na Mjasiliamali,Guochuan Lai.
Guochuan Lai
Wakati hiohuo Mwenyekiti wake Peace ametangaza kuachana na wadhifa huo alioushikilia kwa kipindi cha miaka 14 na nafasi yake itachukuliwa na John Williams kama Mwenyekiti mpya wa klabu.
John Williams
Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyowekwa hadharani kuhusu kiasi cha pesa kilichotolewa kuinunua klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini England.
West Bromwich Albion inakuwa klabu ya tatu kumilikiwa na wawekezaji toka China baada ya Aston Villa na Wolves.
0 comments:
Post a Comment