728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 05, 2016

    HII HAPA RATIBA YOTE YA MICHEZO YA HATUA YA MTOANO LIGI YA MABINGWA ULAYA,MAN CITY YAPEWA WAROMANIA

    Nyon,Uswisi.

    RATIBA ya hatua ya mtoano ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League Play Offs imepangwa mchana huu huko Nyon,Uswisi.

    Katika ratiba hiyo miamba wa Uingereza,Manchester City,wamepangwa kuvaana na Steaua Bucharest ya Romania.

    AS Roma watavaana na Porto huku Borussia Monchengladbach wakipangwa na Young Boys ya Uswisi.

    Wakati huohuo Villarreal wakikutanishwa na Monaco huku miamba wa Uholanzi Ajax wakipewa miadi ya kukutana Rostov.

    Michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa Jumanne Agosti 16 na Jumatano Agosti 17.Marudiano itakuwa Agosti 23 na 24.

    Washindi 10 wa hatua ya mtoano (play-offs) wataungana na timu nyingine 22 zilizokuwa zimefuzu moja kwa moja ili kupangwa katika hatika hatua ya makundi.

    Michezo ya hatua ya makundi (Group Stages) itapangwa Agosti 25 huko Monaco,Ufaransa.

    Ratiba Kamili.

    Ludogorets v Viktoria Plzen
    Celtic v Hapoel Be'er-Sheva
    FC Copenhagen v APOEL
    Dundalk v Legia Warsaw
    Dinamo Zagreb v Salzburg
    Steaua Bucharest v Manchester City

    Porto v Roma
    Ajax v Rostov
    Young Boys v Borussia Monchengladbach
    Villarreal v Monaco

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII HAPA RATIBA YOTE YA MICHEZO YA HATUA YA MTOANO LIGI YA MABINGWA ULAYA,MAN CITY YAPEWA WAROMANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top