Yannick Bolasie
Bolasie:Crystal Palace imekubali dau la £25m kutoka Everton kwa ajili ya kumuuza winga wake Yannick Bolasie.Bolasie,27,alijiunga na Crystal Palace mwaka 2012 akitokea Bristol City kwa dau la £350,000.(ESPN)
Gabriel:Arsenal imeripotiwa kuongeza kasi katika mbio zake za kusaka mlinzi mpya hii ni baada ya mlinzi wake wa kati Gabriel Paulista,26,kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane baada ya kuumia enka.(TeamTalk)
Icardi:Kocha mpya wa Inter Milan Mholanzi,Frank de Boer,amevitaka vilabu vyote vinavyomtaka mshambuliaji wake,Mauro Icardi,23,kuachana na mpango huo kwani nyota huyo wa zamani wa Sampdoria hauzwi.(Gazzetta Dello Sports)
Mangala:Valencia imefungua mazungumzo na Manchester City ili kuangalia uwezekano wa kumsajili mlinzi Eliaquim Mangala (25) kama mbadala ya mlinzi Shkodran Mustafi anayewindwa na Arsenal.(Daily Mail)
Frimpong:Kiungo wa zamani wa Arsenal,Mghana Emmanuel Frimpong,24,amesaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na klabu ya Arsenal Tula akitokea klabu ya FC Ufa.(The Sun)
Baston:Swansea City imekubali kutoa dau la £17m ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa na klabu hiyo kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid,Roja Baston.(London Evening Standard)
Benteke:Baada ya kushuhudia ofa yake ya £25m ikikataliwa Crystal Palace imerejea tena katika meza ya mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya kuhakikisha inamsajili mshambuliaji,Christian Benteke,mwenye thamani ya £32m.(The Sun)
Ghezzal:West Ham haionyeshi dalili za kuchoka katika kipindi hiki cha usajili hii ni baada ya jioni ya leo kuripotiwa kutuma ofa ya €8 kwenda Lyon kwa ajili ya kumsajili winga mwenye asili ya Algeria,Rachid Ghezzal,ambaye pia anawindwa na Everton.(GFFN, via L’Equipe)
Lacazette:Olympique Lyon imepania kuhakikisha staa wake Alexandre Lacazette,25, haondoki klabuni hapo na tayari imemuandalia mkataba mnono utakaomwesha kuvuna zaidi ya £6.5m kama jumla ya mshahara wa mwaka mzima.(London Evening Standard)
0 comments:
Post a Comment