728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 10, 2016

    REAL MADRID YATOKA NYUMA NA KUTWAA UEFA SUPER CUP


    Trondheim,Norway.

    IKICHEZA bila ya mastaa wake Cristiano Ronaldo,Gareth Bale na Toni Kroos,Real Madrid imetoka nyuma na kutwaa ubingwa wa Uefa Super Cup baada ya kuichapa Sevilla kwa jumla ya mabao 3-2 katika mchezo mkali uliochezwa Jumanne Usiku katika uwanja wa Lerkendar Stadion huko Norway.

    Shujaa kwa upande wa Real Madrid alikuwa ni mlinzi wake wa kulia,Dani Carvajal,aliyefunga bao la ushindi dakika ya 119 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Sevilla na kufumua mkwaju uliomshinda mlinda mlango,Federico Rico,na kutinga wavuni.


    Dani Carvajal

    Mabao mengine ya Real Madrid yamefungwa na Marco Asensio kwa mkwaju mkali dakika ya 21' pamoja na nahodha Sergio Ramos kwa kichwa dakika ya 92.

    Sevilla imepata mabao yake kupitia kwa 40Franco Vazquez 40' pamoja na Yevhen Konoplyanka 71.Huo umekuwa ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Sevilla kupoteza katika kipindi cha miaka mitatu.




    VIKOSI

    Real Madrid XI: Casilla, Carvajal, Varane,Ramos, Marcelo, Casemiro, Kovacic, Vazquez,Isco, Asensio, Morata.

    Sevilla XI: Rico, Mariano, Pareja, Carrico,Escudero, Kolo, Iborra, N’Zonzi, Vitolo,Kiyotake, Vietto.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID YATOKA NYUMA NA KUTWAA UEFA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top