Manchester, England.
KIUNGO Mpya wa Manchester United,Paul Pogba,hatakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachoshuka dimbani siku ya Jumapili kucheza na Bournemouth katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England kutokana na kukabiliwa na adhabu ya kukosa mchezo mmoja.
Taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Englan FA mchana huu kupitia twitter imesema Pogba,23,hataruhusiwa kucheza mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano alizozipata wakati akiichezea Juventus ambazo malipo yake huwa ni kukosa mchezo mmoja unaofuata.Awe kwenye kwenye ligi ile ile ama ligi nyingine.
Ikumbukwe mchezaji anapokuwa na adhabu na akahama kutoka ligi moja kwenda nyingine basi huhama na adhabu yake.
Wachezaji wengine ambao kwa mujibu wa FA watakosa michezo ya ufunguzi ya vilabu vyao ni Mlinzi wa Manchester United,Chris Smalling,Kiungo wa Tottenham Mousa Dembele na Mlinzi wa Leceister City,Robert Huth.
0 comments:
Post a Comment