728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 12, 2016

    CAF YABARIKI USAJILI WA KESSY YANGA SC SASA RUKSA KUCHEZA MICHUANO YA SHIRIKISHO


    Cairo,Misri.

    SHIRIKISHO soka barani Afrika Afrika (CAF) limepitisha usajili wa beki mpya wa kulia wa Yanga SC, Hassan Kessy aliyesajiliwa mwishoni mwa Msimu uliopita kutoka kwa watani wao wa jadi,Simba SC.

    Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari iliyochapishwa kwenye Tovuti rasmi ya CAF Usiku wa kuamkia leo,CAF imetoa orodha ya wachezaji wote waliopitishwa katika usajili mdogo wa hatua ya makundi ya michuano ya Afrika– Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

    Taarifa hiyo imeonyesha kuwa wachezaji wote wapya watano wa Yanga wamepitishwa na kupewa leseni za kucheza mechi za Kundi A, zinazoelekea ukingoni ikiwemo ya kesho Jumamosi ambayo Yanga watacheza na MO Bejaia ya Algeria uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    Wachezaji hao ni Obrey Chola Chirwa,Juma Hassan Mahadhi, Benno David Kakolanya, Hassan Khamis Ramadhan ‘Kessy’ na Vicent Andrew Chikupe.

    Orodha/taarifa hii hapa!!



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YABARIKI USAJILI WA KESSY YANGA SC SASA RUKSA KUCHEZA MICHUANO YA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top