728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, August 12, 2016

    CHELSEA YATOA MMOJA KWA MKOPO KUPISHA UJIO WA LUKAKU


    Amsterdam,Uholanzi.

    MSHAMBULIAJI Kinda wa Burkina Faso,Bertrand Traore ameihama Chelsea mchana wa leo na kujiunga na Ajax Amsterdam ya Uholanzi kwa mkopo wa msimu mmoja.

    Ajax Amsterdam imeamua kumsajili Traore ili kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mshambuliaji wake wa zamani,Arek Milik,aliyehamia Napoli kwa ada ya £30m.

    Hii ni mara ya pili kwa Traore kutua ligi ya Uholanzi kwa mkopo.Mara ya kwanza ilikuwa ni kati ya mwaka 2013-15 ambapo aliicheza Vitesse Arnhem kwa mafanikio kwani katika michezo 36 aliyocheza alifanikiwa kufunga mabao 16.

    Wakati huohuo taarifa kutoka England zimesema Chelsea imemtoa Traore kwa mkopo ili kujisafishia njia ya kumsajili Mshambuliaji wa Everton,Romelu Lukaku kwani kisheria klabu hiyo ya Stamford Blidge ingepaswa Kupunguza mchezaji mmoja asiye Muingereza ili iruhusiwe kuongeza mwingine.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YATOA MMOJA KWA MKOPO KUPISHA UJIO WA LUKAKU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top