Dar es Salaam,Tanzania.
YANGA SC imeendelea kusuasua katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Medeama FC ya Ghana katika Mchezo Mkali wa Kundi D uliochezwa katika Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam.
Yanga SC ndiyo waliokuwa wa Kwanza kupata bao la kuongoza baada ya Donald Ngoma kufunga bao dakika ya 2 tu ya mchezo.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Medeama FC ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kusawazishia dakika ya 17 kupitia kwa Bernard Danso na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Kwa matokeo hayo Yanga SC imeendelea kubaki mkiani mwa kundi A kwani licha ya kucheza michezo mitatu imefanikiwa kupata pointi moja pekee.
Timu hizo zitarudia Julai 26 huko Sekondi-Tokoradi,Ghana.
0 comments:
Post a Comment