728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, July 16, 2016

    LIGI YA MABINGWA AFRIKA:ZESCO UNITED YAENDELEZA UBABE NYUMBANI YAICHAPA ASEC 3-1

    Ndola,Zambia.

    Zesco United ya Zambia imefufua matumaini ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya jioni ya leo kuifumua ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Levy Mwanawasa huko Ndola,Zambia.

    Mpaka mapumziko Zesco United ilikuwa kifua mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Jackson Mwanza na John
    Ching'andu.

    Kipindi cha pili kilianza kwa wageni ASEC Mimosas kuja juu na kufanikiwa kupata bao la kufutia machozi baada ya Dao Youssouf kufunga katika dakika ya 75 ya mchezo.Dakika ya 78 ,Idriss Mbombo,aliihitimisha kalamu ya mabao baada ya kuifungia Zesco United bao la tatu na kufanya mchezo uishe kwa wenyeji Zesco United kushinda kwa mabao 3-1.

    Ushindi huo umeipeleka Zesco United mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi sita sawa na Wydad Casablanca ambayo baadae itavaana na Al Ahly.

    Zesco United na Asec Mimosas zinatarajiwa kurudiana tena Julai 27 huko Abidjan katika dimba la Stade Robert Champroux.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA AFRIKA:ZESCO UNITED YAENDELEZA UBABE NYUMBANI YAICHAPA ASEC 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top