728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 06, 2016

    TAMBWE AJA NA JIPYA KUHUSU UGOMVI WAKE NA DONALD NGOMA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amissi Tambwe,amesema amemaliza bifu na Donald Ngoma na kuahidi kutoa ushirikiano utakaowezesha timu hiyo kupata pointi tatu katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana.

    Nyota hao tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya Yanga walipigana wakati timu ikiwa kambini nchini Uturiki na kuwekeana bifu, hali iliyomfanya kocha Hans van der Pluijm kuingilia kati ili kusuluhisha ugomvi wao.

    Akizungumza jana, Tambwe ambaye aliumizwa vibaya na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu, alisema amemsamehe Ngoma na sasa anaungana naye ili kusaidia ushindi dhidi ya Medeama watakaovaana Juni 16, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

    “Ugomvi wetu umekwisha sasa sina tatizo na Ngoma kwa sababu ni mchezaji mwenzangu ambaye tutashirikiana kwa pamoja kusaka ushindi katika mchezo dhidi ya Medeama ili kujiwekea mazingira
    mazuri zaidi.

    “Mashabiki waondoe wasiwasi maana nafikiri jambo hili liliwaumiza sana na walikuwa wanasubiri kwa hamu kusikia tumefikia mwafaka, kwa sasa tutacheza kwa ushirikiano wa hali ya juu ili tufikie
    malengo yetu,” alisema Tambwe.

    Ugomvi wa mastraika hao ulipokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Yanga,kutokana na kutokea kipindi ambacho timu inakabiliwa na mechi ngumu za kimataifa na ushirikiano wao uwanjani ni muhimu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAMBWE AJA NA JIPYA KUHUSU UGOMVI WAKE NA DONALD NGOMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top