728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, July 06, 2016

    BAADA YA MESSI,KOCHA NAE AIKIMBIA ARGENTINA SIRI KIBAO ZAVUJA

    Buenos Aires,Argentina.

    KAMBI ya Timu ya Taifa ya Argentina imeendelea kupata mapingo makali makali tangu ilipochapwa na Chile katika Fainali za Copa America siku kumi zilizopita nchini Marekani.

    Nahodha Lionel Messi alianza kuishitua dunia kwa kutanzanga kuachana na timu hiyo,akaja Rais wa chama cha soka,Luis Segura na sasa aliyekuwa Kocha wake Mkuu,Gerardo Martino,kutangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo kuanzia Jana Jumanne.

    Martino,53,amefikia uamuzi huo kwa kile kinachodaiwa kuwa kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Newell Old Boys hakuwa akipewa sapoti ya kutosha na chama cha soka cha nchi hiyo AFA.

    Imedaiwa pia Martino alikuwa akifanyishwa kazi bila ya kulipwa mshahara wake.Mpaka anabwaga manyanga Martino ameripotiwa kuwa hajalipwa mishahara yake kwa kipindi cha miezi sita sasa.

    Sababu nyingine iliyodaiwa kumbwagisha manyanga Martino ni kwamba licha ya kupewa jukumu la kuiongoza Argentina katika michuano ya mwaka huu ya Olyimpiki lakini ameshindwa kupata wachezaji wa kuunda kikosi hicho hii ni baada ya vilabu vya nchi hiyo vikiongozwa na River Plate pamoja na Boca Juniors kutia ngumu kutoa ruhusa kwa wachezaji wao kushiriki katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake nchini Brazil mwezi hapo Agosti mwaka huu.

    Martino alianza kuinoa Argentina mwaka 2014 baada ya kuisha kwa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil na Ujerumani kuibuka mabingwa kwa kuichapa Argentina kwa bao 1-0.

    Akiwa na Argentina,Martino, aliiongoza Albiceleste kucheza jumla ya michezo 29,akishinda 19,sare 7 na kufungwa mara tatu dhidi ya Chile na Ecuador.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA MESSI,KOCHA NAE AIKIMBIA ARGENTINA SIRI KIBAO ZAVUJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top