Genk,Ubelgiji.
Timu ya K.R.C. Genk anayochezea mtanzania , Mbwana Samatta imejiweka katika mazingira mzuri ya kucheza Europa Ligi baada ya usiku wa leo kuibuka na ushindi wa bao 2 – 0 dhidi ya Buducnost Podgorica ya Montenegro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya mchujo Mchezo huu uliopigwa katika uwanja wa nyumbani wa Genk uitwao Cristal Arena mjini Genk , ulianza kwa kasi huku Genk wakipata penalti ya mapema dakika ya 17 ya mchezo , ambapo Neeskens Kebano aliweza kuandika bao la kwanza.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Genk walikua wanaongoza kwa bao 1 – 0.
Kipindi cha pili kilikua na vuta ni kuvute hadi hapo dakika ya 79 ambapo Mbwana Samatta alipigilia msumari wa ushindi .Hadi mchezo unamalizika matokeo yalikua 2 – 0 .
Samatta leo alicheza mshambuliaji pekee hadi dakika ya 76 ambapo mshambuliaji pacha wake anayehusishwa na usajili kwenda Nottingham Forest , Nikos Karelis alipoingia .
Timu hizi mbili zitarudiana
alhamisi ijayo huko Montenegro.
0 comments:
Post a Comment