728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, October 04, 2015

    TUMECHOKA:RASMI LIVERPOOL YAMTUPIA VIRAGO BRENDAN RODGERS,KLOP,ANCELOTTI WAJIANDAA KUCHUKUA MIKOBA

    Liverpool,England.

    Brendan Rodgers siyo kocha wa Liverpool tena hii ni baada ya kutupiwa virago jioni ya leo pale alipoiongoza klabu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na Everton katika muendelezo wa mshikemshike wa ligi kuu England.

    Rodgers ametupiwa virago baada ya wamiliki wa klabu hiyo kampuni ya Fenway Sports Group inayoongozwa na Mike Gordon kuona kuwa kocha huyo kwasasa hana jipya na siyo mtu sahihi tena wa kuipeleka mbele miamba hiyo ya zamani ya Ulaya.

    Mpaka anatupiwa virago leo,Rodgers alikuwa ameshinda mchezo mmoja pekee katika michezo tisa ambayo Liverpool imecheza msimu huu huku ikiwa imefanya usajili wa kutisha kwa kuwasajili nyota kama James Milners,Christian Benteke,Joe Gomes,Roberto Firmino,Nathaniel Cylne na Bodgan.

    Rodgers alijiunga na Liverpool mwaka 2012 akitokea Swansea City licha ya kutumia kitita cha £291m hakufanikiwa kushinda taji lolote lile akiwa na Liverpool zaidi ya kuirejesha klabu hiyo katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita ambapo ilitolewa mapema.

    Wakati huohuo makocha Jurgen Klopp na Carlo Ancelotti wameanza kutajwa kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers na huenda mmoja wao akatangazwa kuwa kocha mpya wa Liverpool hivi karibuni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TUMECHOKA:RASMI LIVERPOOL YAMTUPIA VIRAGO BRENDAN RODGERS,KLOP,ANCELOTTI WAJIANDAA KUCHUKUA MIKOBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top